Ismail Jussa, mmoja wa viongozi wa ACT Wazalendo ambao walishambuliwa na kujeruhiwa vibaya na vyombo vya dola, amerejea nyumbani Zanzibar akitokea nchini Kenya alikokwenda kwa ajili ya matibabu. Jussa amepokewa na ndugu na marafiki kwa shangwe kubwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume.