Duration 1:34

Familia ya Koitalel Arap Samoei yataka juhudi za shujaa huyo zipewe kipaumbele

2 209 watched
0
21
Published 20 Oct 2020

Familia ya Koitalel Arap Samoei shujaa aliyepigania uhuru sasa inataka fidia kutokana na juhudi alizochangia kwa kuhakikisha taifa linapata ukombozi kwa kupinga uongozi wa kiimla. Familia ya koitalel ilikuwa ikizungumza wakati wa hafla ya kumkumbuka miaka 115 tangu kuuawa kwake kinyama katika eneo bunge la nandi hills viongozi waliohudhuria hafla hiyo wakiongozwa na magavana stephen sang wa nandi, alex tolgos wa elgeyo marakwet na stanley kiptis wa baringo wakiunga semi za familia na kutaka serikali kuu kuingilia kati na kuona familia za waliopigania uhuru wamepata fidia kwani wanaoonekana kufaidi ni wale walioshirikiana na wale waliowatesa. Tayari chuo kikuu cha koitalel samoei kimejengwa kwa ukumbusho wa shujaa huyo

Category

Show more

Comments - 1