Duration 3:19

WAGANGA WA TIBA ASILI MBEYA MBARONI KWA TUHUMA ZA UTAPELI.

458 watched
0
5
Published 4 Jun 2021

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya SACP Ulrich Matei amesema Jeshi la Polisi Mkoani hapa Lina washikilia watu watatu waganga wa tiba asili kwa tuhuma za kumtapeli mwalimu mstaafu Wa shule ya msingi Wimba kiasi cha shilingi millioni 20. kamanda Matei amesema watuhimiwa hao wamekamatwa katika msako ulio fanywa maeneo ya nanenane Jijini Mbeya na kufanikiwa kuwakamata watu hao watatu. Mwalimu Samweli Mbwambo amesema watu hao alifahamiana nao kwaajili ya kwenda kupata matibabu ya kifaga na tarehe 20 desemba mwaka Jana na baadae Waka mshawidhi kumlahisishia kupata mafao yake. Kwa upande wake mganga watiba asili Jobu Masangano amesema mwalimu huyo alienda kupata matibabu yeye na mke wake akiwa na matitizo ya kifafa na mkewe akiwa na matatizo ya uzazi. Masangano amesema katika makubaliano yao mwalimu huyo aliahidi kutoa zawadi kwa mganga huyo kama wakipona matatizo hayo yaliyo wasumbua mda mrefu ambapo baada ya kupokea mafao yake akawapelekea kiasi cha shilingi millioni 14.

Category

Show more

Comments - 1